Kinana Awaaga Wabunge wa CCM kwa Maneneo Mazito "Ninyi Ndiyo Mtakaonihukumu"

Nilijituma Kazi kwa Maarifa Yangu Yote Ninyi Ndiyo Mtakaonihukumu- Kinana
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewaaga rasmi wabunge wa chama hicho huku akiwataka kutokubali mgawanyiko ndani ya chama pamoja na bunge kwa tofauti ndogo ndogo.


Kinana amesema hayo katika halfa iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga na kumkaribisha Katibu Mkuu, Dk Bashiru Ally iliyofanyika katika hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Akitoa hotuba yake ya kuaga wabunge hao, Kinana amesema kwamba kama wabunge wa chama kimoja wanapaswa kutumia kanuni, kubishana kwa hoja na siyo vitisho au mambo mengneyo."

"Tusirushusu tofauti za maoni yetu kuwa chanzo cha mgawanyiko wa chama na bungeni, Mbishane kwa hoja na siyo vitisho. Kanuni za CCM zinapaswa kufanyiwa marekebisho kwani ziliandaliwa toka miaka 20 iliyopita. Zinapaswa kurekebishwa ili kuendana na mahitaji ya sasa" Kinana.

Aidha Kinana ameenda mbali zaidi na kusema "Nilijitahidi kujitolea, kufanya kazi, kujituma kwa maarifa yangu yote na ninyi ndio mtakaonihukumu kama nilifanya kazi ipasavyo. Kama kuna upungufu uliojitokeza nakiri kwamba ni wangu binafsi na kama kuna mafanikio hayakuwa na maarifa na juhudi zangu bali ni matokeo ya juhudi za wana CCM na wabunge wote".

Aidha Katibu Mkuu huyo Mstaafu amewahusia Wabunge hao  kuendelea kujenga imani kwa wananchi kupitia serikali iliyopo madarakani ambayo inaongozwa na CCM.

“Serikali ikitimiza ahadi zake kwa wananchi, itaendelea kuaminika na serikali ikipokea matatizo ya wananchi na kutimiza yale wanayoyataka, watafarijika na mtaendelea kuchaguliwa kwa idadi kubwa na mwisho wa siku CCM itapata ridhaa ya kuendelea kuongoza.”

Pamoja na hayo Kinana amewaambia Wabunge hao wa CCM kwamba ameamua kwenda kupumzika.

“Kuna wakati wa kuchukua dhamana na kukubali kuondoka, kuna wakati wa kukubali kazi moja na kwenda kufanya nyingine, kuna wakati wa kufanya kazi na kuna wakati wa kupumzika. Nimeamua kwenda kupumzika,” amesema.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad