HISPANIA: Kocha wa Real Madrid, Mfaransa Zinedine Zidane leo Mei 31, 2018 ametangaza kujiuzulu kufundisha klabu hiyo kwa msimu ujao ikiwa ni siku tano baada ya kuipa ubingwa wa UEFA Champions League mara ya 3 mfululizo.
Zidane anaondoka klabuni hapo kwa heshima baada ya kuitumikia kwa miaka miwili. Mfaransa huyo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo.
Mkongwe huyo wa soka mwenye miaka 45, baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa ilikuwa inatabiriwa angeongezewa mkataba hadi mwaka 2020. Hata hivyo awali kulikuwa na presha kubwa kutoka uongozi wa Madrid kutokana na kutofanya vyema kwenye La Liga msimu huu ulioisha.
Makocha Arsene Wenger na Antonio Conte ni miongoni mwa wanaotajwa kumrithi Zidane, huku Conte akipewa nafasi kubwa Zaidi.
Zidane alimrithi kocha Rafael Banitez Januari 2016 na msimu huo huo aliipa taji la Ligi ya Mabingwa timu hiyo.
Zidane ameitumikia Madrid tangu (2016-18)
UEFA Champions League🏆🏆🏆
UEFA Super Cup🏆🏆
Club World Cup🏆🏆
Spanish Super Cup🏆
Liga🏆