Kitendo Cha Uhuru Kenyatta Kumuomba Rais Msamaha Kwa Aliyomtendea Wakati wa Uchaguzi Tanzania Tuna Jifunza Nini?

Kusema kweli kwa kitendo alichofanya Uhuru Kenyatta cha Kumuomba Rais Msamaha live bila kujali nini kitaendelea baada ya hapo katika uwanja wa siasa Kenya kinahitaji pongezi na labda kujifunza. Haya ndio mambo ambayo nchi yetu ilikuwa inasifika sana.

Tanzania ilikuwa ndio nchi ya Africa iliyokuwa kimbilio kwa wale wenye magomvi na kutokuelewana wakaja Tanzania kupatanishwa. Vyama vya wapigania Uhuru kama ZANU na ZAPU viliweza unganishwa kwa juhudi za Mwalimu Nyerere ikatoka Patriotic Front nakumbuka Mwalimu pia alijaribu sana kuweza kuunganisha ANC na PAC vyama vya ukombozi wa Afrika kusini kipindi kile lakini naona pale hakufanikiwa lakini juhudi zilifanyika.

Na najua wako wengine wengi wanaweza kuja na mifano mingi ya kuonyesha jinsi gani nchi yetiu ndio ilikuwa muubiri na mtekelezaji wa dhana ya Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu. Tuliimba hizi nyimbo shule za msingi na kweli tulifanikiwa sana kujenga nchi moja yenye mshikamano usiojali dini, ukabila au rangi. Nafikiri hili tunahitaji kuliweka kama ndio msingi Mama kadri tunavyozidi kwenda mbele katika mapambano ya kujenga Tanzania yetu.

Leo Kenya wamegundua kuwa utengano ni udhaifu. Watanzania tufungue macho na masikio tunayaone na kuyasikia haya na bila kuyapuuzia, kwa sababu ukweli hata siku moja haupuuzwi kama una nia ya kweli ya kuboresha na kujifunza.

VIDEO:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad