Kuhusu Kutumia Madawa ya Kulevya Chidi Benz Anena Haya "Siwezi Kujutia Chochote Kilichonipata"

Kuhusu Kutumia Madawa ya Kulevya Chidi Benz Anena Haya "Siwezi Kujutia Chochote Kilichonipata"
Rapper huyo ameeleza kuwa hiyo ni kutokana na mashabiki wake wamekuwa naye bega kwa bega kwa kila jambo ambalo anapitia.

“No! no!, tusiongelee mambo ya madawa maisha ndio yapo hivyo, hamna kitu ninachojutia. Siwezi kujutia nilikolabo na wasanii, siwezi kujutia yaliyonikuta, siwezi kujutia mabadiliko yangu, siwezi kujutia chochote kilichonipata,” amesema.

“Zaidi naona nikijutia mashabiki wangu wataona Chidi vipi why wewe hujutie wakati sisi tunaendelea kukupenda hadi leo. Ukitangaza show TMK unajaza, Morogoro, Singida unajaza, unajutia nini,” Chidi Benz ameiambia Wasafi TV.

Katika hatua nyingine Chidi Benz amesema karibia studio zote alizokwishafanya kazi ana nyimbo zaidi ya saba hivyo muda wowote atatoa wimbo ila kuna ngoma aliyofanya na Mr. T Touch ndio ipo katika nafasi nzuri zaidi kutoka. Utakumbuka wimbo wa mwisho kwa msanii huyo kutoa official ni Muda aliyomshirikisha Q Chief.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad