Kuhusu Picha Tata za Uwoya Dogo Janja Asema Haya "Irene ni Staa Mapaparazi Hawakoso"


Kuhusu Picha Tata za Uwoya Dogo Janja Asema Haya "Irene ni Staa Mapaparazi Hawakoso"
Msanii Dogo Janja amefunguka kuhusu kusakamwa kwa mke wake, Irene Uwoya kufuatia picha zake alizoweka kwenye mitandao ambazo kwa asilimia kubwa ziliacha wazi umbile lake.

Dogo Janja amesema si kweli mke wake alikuwa uchi kama inavyoelezwa bali ni vazi la kawaida kwa maeneo ya ufukweni, pia mke wake ni staa hivyo mambo kama hayo ni kawaida kutokana na kufuatiliwa na mapaparazi.

“Irene kuvaa vile kwanza alikuwa ufukweni, Irene ni staa popote anapokuwa lazima kuwe na kamera, paparazi hawakosi, kwa hiyo popote wanapoenda paparazi kwao ni content, so alikuwa pale beach kabiga picha kavaa nguo hakuwa uchi,” amesema.

Si Dogo Janja pekee aliyemkingia kifua Irene Uwoya kutokana na picha hizo, bali hata mwingizaji wa filamu Bongo, Shamsa Ford alieleza kuwa Irene alikuwa sahihi kuvaa vile kutokana na eneo husika (ufukweni).

Top Post Ad

Below Post Ad