Mrembo huyo miezi miwili iliyopita alitangaza kwamba amedundwa na aliyekuwa mume wake, Henry Kileo na baadaye mashabiki pamoja na wadau mbalimbali kumponda kutokana na tukio la kujitangaza.
Joyce Ijumaa hii alikuwa EFM redio ambapo amefunguka mambo mbalimbali pamoja na kudai kuna wanawake wanaharakati wanadudwa na waume zao lakini wanashindwa kuweka uovu huo hadharani.
“Kuna wanaharakati wanaojiita wanaharakati (Wanawake) wanapigwa, kudhalilishwa na kufanyiwa matendo mengi ya udhalilishaji lakini hawasemi,” alisema mwanamke kupitia kituo hicho cha redio.
Aliongeza, “Kuwa kioo cha jamii haimaanishi ufiche yakwako yanayokuumiza. Mimi kama superwoman Joyce Kiria nimekua mfano wa kuwasemea wanawake wengine wanao nyanyasika”
Baada ya tukio hilo mwanaharakati huyo aliachana na mume wake huyo na baadaye kuonekana katika kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ya wanawake waliotelekezwa na waume zao lakini alivyofuatwa alitaa kuzungumza kilichompeleka ofisini hapo.