Kupiga Picha Kuonyesha Nguo za Ndani za Mwanamke Sasa ni Kosa


Tabia hiyo inazidi kukua hasa kutokana na teknolojia inayowezesha mtu kuweka kamera miguuni mwa mwanamke akiwa ameishikilia kwa fimbo maalum.

Tabia ya wanaume kupiga picha maeneo ya kike ya mwanamke kwa kuvizia, maarufu kwa jina la upskirting, huenda ikapigwa marufuku nchini Uingereza, kwa mujibu wa sheria inayojadiliwa bungeni.

Mtu atakayepatikana na hatia ya kupiga picha hizo kwa nia ya kuonyesha nguo za ndani za mwanamke, anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka miwili jela.

"Tabia hii ni uvamizi wa faragha unaomuacha aliyefanyiwa hivyo kujisikia vibaya na amedhalilishwa," waziri mdogo wa sheria, Lucy Frazer alisema, akibainisha msimamo wa serikali kuunga mkono muswada uliowasilishwa na mbunge wa upinzani, Wera Hobhouse.

Watakaopatikana na hatia ya kupiga picha maeneo ya siri ya mwanamke, watachukuliwa wamefanya kosa la shambulizi la kijinsia.

Kwa sasa baadhi ya makosa ya aina hiyo yanashughulikiwa chini ya sheria ya utovu wa heshima, lakini wanaharakati wanasema si matukio yote yanayoweza kushughulikiwa na sheria hiyo.

Mmoja wa wanaharakati hao, Gina Martin alianzisha madai kwa njia ya mtandao baada ya polisi kukataa kumshtaki mtu mmoja aliyemtuhumu kuwa alimpiga picha kwa kutumia simu yake wakati wa tamasha la muziki zikionyesha nguo zake za ndani na baadaye picha hiyo kuchukuliwa kuwa batili.

"Hizi ni habari kubwa," alisema Martin akizungumzia mpango huo wa Serikali ya Uingereza kuharamisha upigaji picha hizo.

"Sasa natumaini tunaweza kuifikia haki kwa waathirika wote kwa sababu wanasiasa wamesikiliza."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad