Lupita Nyong’o Azidi Kupeta.... Kupewa Tuzo Kubwa ya Heshima Hollywood

Lupita Nyong’o Azidi Kupeta....  Kupewa Heshima Kubwa Hollywood
MDADA mwenye asili ya Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o amezidi kupeta ambapo safari hii anatarajiwa kupewa tuzo kubwa ya heshima ndani ya eneo la Hollywood iitwayo Hollywood Walk of Fame.

Tayari majina ya watu maarufu watakaopewa heshima hiyo yameshaanikwa. Lupita anaugana na Alan Arkin, Kristen Bell, Daniel Craig, Tyler Perry na wengine wengi.

Hii ni heshima kubwa kupewa kwani wapo mastaa ‘a list’ kama vile Will Smith, Brad Pitt, Angelina Jolie na Madonna ambao miaka nenda rudi hawajawahi kuambuliwa kupewa heshima hiyo.

Hata hivyo, siku rasmi ya kusherehekea heshima hiyo bado haijatangazwa japokuwa inafahamika kuwa itakuwa mwakani.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad