Madeni ya Jeshi yatua Bungeni...Spika Ndugai Atoa Maagizo

Bungeni
Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka wabunge wote wanaodaiwa na Jeshi la Kujenga Taifa wahakikishe wanalipa madeni yao haraka iwezekanavyo kwani siku zilizotolewa zinaisha Juni 23 Mwaka huu.

Agizo hilo la Spika limekuja baada ya kusoma tangazo hilo la madeni jana ambapo alisema kuna orodha ndefu ya wabunge wanaodaiwa na kwamba baadhi yao hawana hata fedha za ziada katika posho zao wanazolipwa.

“Mtakumbuka mheshimiwa Rais alitoa agizo hilo Mei 17, aliagiza madeni yote kulipwa ndani ya siku 30 kuanzia siku hiyo, leo naomba wabunge mlipe haraka sana madeni hayo na mwisho ni Juni 23,” alisema Ndugai.

Spika alisema orodha ya wadaiwa ipo mezani kwake na kwamba angetamani kuwataja lakini alishapitia majina yao na amebaini baadhi yao wana mikopo ndani ya Bunge hivyo kwenye mfuko huo hawawezi kukatwa fedha za kulipia madeni

Mei 17 mwaka huu, Rais John Magufuli alitoa mwezi mmoja kwa taasisi za Serikali na watu binafsi wanaodaiwa na Jeshi kuhakikisha wanalipa fedha hizo  ili ziweze kutumika kujenga viwanda vingine ambapo alidai kutolilipa jeshi ni dharau kubwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad