Magdalena Sakaya Amshukia Maalim Seif 'Alizuia Fedha za Ruzuki ili Kukiua Chama cha CUF'

Kaimu katibu mkuu wa CUF upande wa Profesa Lipumba, Magdalena Sakaya amemshukia Maalim Seif na kudai alikuwa na lengo la kukiua chama hicho, ndio maana aliweza kuzuia chama kisipate ruzuku kwa nchi nzima baada ya mgogoro wa mwaka 2016.


Akizungumza kwenye kipindi cha East Afrika BreakFast kinachorushwa na East Afrika Radio, Sakaya amesema chama hicho kimepitia katika wakati mgumu  ambapo fedha zote zilizuiliwa na Maalim Seif kwa kuandika barua kwenda kwenye taasisi zote za kifedha pamoja na serikali kuzuia wasiendelee kutoa ruzuku kwa chama hicho.

Aidha Sakaya ameweka wazi, namna alivyolazimika kupigania hadhi ya chama hicho kwa kuomba upya ruzuku na kulazimika kuchukua mikopo ili kuendesha shughuli za chama,

"Chama cha Wananchi (CUF) shida ni  mtu mmoja, yaani huu mgogoro ni wa mtu mmoja, ambao 'actually' ni ubinafsi na hiki chama ni taasisi sio chama cha Maalim Seif wala Prof. Lipumba, ndio maana kimeweza kuendelea bila hata ya wao, japokuwa lengo la maalim seif lilikuwa ni kuua CUF, lakini bado taasisi yetu imeendelea kuwa imara, hivi tunvyoongea kuna viongozi katika kila kona ya nchi wanasimamia chama", amesema Sakaya.

Akimuongelea Profesa IbrahimLipumba kama Mwenyekiti wa upande wake amesema kwa sasa ameweza kurejesha imani kwa wananchama, katika maeneo mengi nchini, kutokana na ziara yake aliyoifanya, yakuzunguka nakuzungumza na watu, kuwaeleza sababu ya yeye kutangaza kujihudhuru uenyekiti wa chama mwaka 2015.

EATV
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad