Maisha ya Yanga kabla na baada ya kuondoka Manji

Kwenye kipindi cha Sports Xtra cha Jumanne Juni 4, 2018, kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga alizungumza mambo mengi yanayohusu klabu hiyo.

Miongoni mwa mambo ambayo aliyadadavua upana ni maisha ya Yanga kabla na baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji.

Tunashukuru kwa alichofanya Manji katika kipindi chote ambacho alikuwa madarakani na kabla ya kuwa madarakani wakati huo akiwa mdhamini wa klabu, amekuwa ni msaada mkubwa.

Kila mwanachama na mpenzi wa Yanga anajua maisha tuliyokuwa nayo wakati huo, Manji alikuwa mpiganaji na timu iliweza kufanya vizuri kwa kipindi chote ambacho alikuwepo.

Katika kipindi cha hivi karibuni wakati Manji yupo Yanga tuliweza kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kambi mbalimbali hakukuwa na tatizo la kulipa mishara, ilikuwa inalipwa kwa wakati.

Aina ya wachezaji na benchi la ufundi lilikuwa ni zuri sana katika vipindi vyote ambavyo alikuwepo na hakukuwa na dosari.

Tulikuwa na kipindi cha neema kipindi hicho Manji yupo. Alikuwa analipa mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi na secreriat kiasi kisichopungua Tsh. 125M kwa mwezi.

Ishu za usajili kwa wastani tulikuwa tunaweza kusajili wachezaji kwa kiasi cha Tsh. 500 hadi 600M.

Kwa hiyo unaweza kuona ni gape kubwa kwa yeye kutokuwepo ndani ya uongozi na kama mfadhili wa klabu ya Yanga.

Alipotangaza kujiuzuli ilikuwa kama mshtuko  na katika hali ya kawaida huwezi kutafuta njia ya kukimbia badadala yake unajipanga na kutulia ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Tunashirikiana na kamati ya utendaji kwa pamoja na mazingira yaliyoliyopo, tangu Manji ameondoka tulikuwa na deni kama miezi mitatu mapaka leo ni wastani wa miezi 18 ambayo pia nimekuwa nikikaimu nafasi yake.

Katika miezi hiyo 18 uongozi huu uliobaki umeweza kulipa mishahara kwa miezi 16, tuna deni la mishahara ya miezi miwili ambalo tunaendelea kulifanyia kazi kuhakikisha tunakamilisha. Changamoto ni moja, kwamba mishahara ilikuwa haiji kwa wakati katika kipindi chetu lakini kwa kifupi tuna deni la mishahara ya miezi miwili.

Sanga amesema wakati Manji yupo kulikuwa na mfumo kwanza yeye kama Mwenyekiti na mfadhili wa timu alikuwa anaweza kuchangia kwa atakavyoona inafaa kwa wakati huo kwa hiyo alikuwa anasimama kama mwenyekiti na mfadhili wa timu kwa wakati mmoja.

Ndiyo maana waliokuwa wanabeza mpango wa mabadiliko ya uendeshaji alipojaribu kuomba akodishwe nembo ya Yanga wakasema aondoke atakuja mwekezaji mwingine, tangu ameondoka hajaja mtu zaidi ya watu kukimbia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad