Makombe feki ya Kombe la Dunia yakamatwa Argentina, ndani yalikuwa yamejazwa Cocaine na bangi

Makombe feki ya Kombe la Dunia yakamatwa Argentina, ndani yalikuwa yamejazwa Cocaine na bangi (+video) By Godfrey Mgallah | June 25, 2018 - 5:35 pm
Maafisa wa usalama nchini Argentina, wamekamata makombe 8 bandia yenye muonekano sawa na ule wa Kombe la Dunia yakiwa yamejazwa misokoto ya bangi na Cocaine.



Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Makombe hayo 8 yamekamatwa Ijumaa ya wiki iliyopita mjini Isidro Casanova katika jimbo la Greater Buenos Aires.

Makombe hayo kiujumla yalikuwa yamebeba kilo 20 za bangi na kilo 10 za Cocaine na mafurushi kadhaa ya mafataki.

Jeshi la Polisi mjini Isidro Casanova limethibitisha taarifa hizo na tayari watu nane wanashikiliwa kwa tukio hilo na imekadiriwa kuwa kila kombe lilikuwa na mzigo wa Cocaine wenye thamani ya dola $14,819 sawa na tsh milioni 33.

Tazama makombe hayo yakipasuliwa na jeshi la polisi.


Bongo5

Top Post Ad

Below Post Ad