Makonda Jino kwa Jino na wanaowatumikisha watoto kama Kitega Uchumi


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametangaza kuwasaka wananchi wanaotumia watoto wakiwamo wenye ulemavu, yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kama kitega uchumi cha kujipatia kipato kwa kuwafanyisha shughuli mbalimbali ikiwamo kuombaomba mitaani. 


Makonda alitangaza msako huo unaenda sambamba na kuitaka jamii kuwafichua watu hao jana wakati akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa idadi ya watoto wanaoishi na kufanyakazi mitaani, kinyume na sheria iliofanywa na Shirika la kulea watoto yatima la Babawatoto. 

"Nitoe rai kwa jamii na wazazi au walezi wanaowatumia watoto hawa kwa ajili ya kujipatia kipato kuwa hawako salama kwa sababu nitaanza msako wa kuwakamata hivyo ni vyema jamii ikaanza kuwaripoti mapema. Zaidi wanawakosesha haki yao ya msingi ya kupata elimu bure inayotolewa na serikali," alisema Makonda. 

Utafiti huo umebaini Mkoa wa Dar es salaam pekee una jumla ya watoto 3,312 wanafanya kazi mitaani na kati ya hao watoto 2,984 walionekana wakifanya kazi nyakati za mchana na 328 wanafanya kazi nyakati za usiku. 

Aidha RC Makonda amewaonya watu wenye tabia ya kuwapatia ombaomba fedha barabarani kuwa Ndio wanaohalalisha uwepo wa watu hao ambapo amesema Kama mtu anataka kweli kusaidia waishio maisha magumu wapeleke misaada kwenye vituo vilivyopo kwa mujibu wa sheria kwakuwa vituo hivyo vinafuatilia maenendo ya watoto kitabia, elimu na matibabu ambapo ukimpa pesa mtoto barabarani unatengeneza mazingira ya kuwa na fedha ambayo hana uhalali nayo na anapokuwa mtu mzima anakuwa mkabaji,mporaji na kuchoma visu watu wasio na hatia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad