Mali za Mpinzani wa Rais Kagame Zapigwa Mnada

Mpinzani wa Rais Kagame Mali Zake Zapigwa Mnada
Leo June 19, 2018 kutoka nchini Rwanda taarifa zinasema mali za mpinzani wa rais wa Rwanda, Paul Kagame zimepigwa mnada mara baada ya mamlaka ya ukusanyaji wa kodi nchini humo kuzizuia ikidai kuwa zinadaiwa kodi ya kiasi cha dola milioni 7.

 ambaye yuko kizuizini alizuiwa kuwania urais mwaka uliopita na baadaye kukamatwa kwa madai ya uchochezi na kutaka kufanya mapinduzi ya serikali.

Halmashauri ya ukusanyaji mapato nchini Rwanda imeuza mashine za kuchakata tumbaku kwa takriban dola milioni 2 katika hatua ya kulipia kodi inayodaiwa familia hiyo ambayo inaripotiwa kudaiwa dola milioni 7.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad