Mamake kiongozi wa Boko haram Abubakar Shekau amezungumza kwa mara ya kwanza akiambia idhaa ya VOA ya Marekani kwamba mwanawe amewaletea watu wengi matatzio na kwamba hajamuona kwa kipindi cha miaka 15.
''Namuombea mungu amuonyeshe njia nzuri'', aliambia kituo hicho cha habari
Falmata aliongezea:
Kweli ni mwanangu na kila mama humpenda mwanawe lakini tuna tabia tofauti. Ameleta matatizo mengi kwa watu wengi. Nitakutana naye wapi ili nimwambie kwamba mambo anayofanya ni mabaya.
Alichukua tabia tofauti na kuondoka. Sijui hii ni tabia gani?. Ni Mungu pekee anayejua. Nitakutana naye wapi ili nimwambie kwamba vitu anavyofanya sio vizuri?
Kundi la wapiganaji wa Boko Haram lilianza vita dhidi ya Serikali ya Nigeria 2009 kwa lengo la kuweka taifa la Kiislamu Afrika Magharibi.
Kundi hilo linaloangazia kwa sana Kaskazini mwa Nigeria limesababisha vifo vya watu 20,000 huku watu wengine milioni mbili wakisalia bila makao.
Likiongozwa na Abubakr Shekau, boko haram liliahidi kutii kundi la wapiganjai wa Islamic State mnamo mwezi 2015.
Mwezi Agosti 2016, kundi hilo lilivunjika huku kanda ya video ya IS ikitangaza kuwa mahala pake Shekau pamechukuliwa na Abu Musab al-Barnawi, ambaye anaaminika kuwa mwana wa mwanzilishi wa kundi la Boko Haram.
Bwana Shekau alipinga wazo hilo akisisitiza kuwa bado yuko kileleni mwa kundi hilo.
''Sijui kama amefariki ama ni mzima'', alisema Falmata.
''Ni Mungu anayejua''