Mambo 50 ya kisaikolojia yatakayokuacha kinywa wazi


Mambo 50 ya kisaikolojia yatakayokuacha kinywa wazi
Hii ni kwel hata kama ulikua hujui kubali tu, maana ndio ukweli uliopo.

1. Mtu hufanya ishara nyingi za mikono akiwa anazungumza ukweli. Azungumzae uongo mikono yake huwa imetulia zaidi.

2. Sikiliza kwa makini namna mtu anavyozungumzia watu wengine akiwa na wewe, na ndivyo atakavyokuzungumzia wewe akiwa na watu wengine.

3. Ndoto zako zinabeba ujumbe mhimu sana. Asilimia 70 ya ndoto zako zina ujumbe wa siri.

4. Kwa kawaida watu huwa waaminifu na wakweli mwili ukiwa umechoka, na ndio sababu hutubu na kutoa siri zao kwenye mazungumzo yatekeayo usiku wa manane,

5. Ukihisi mtu au watu wanakuangalia, angalia saa au muda kama unataka kujua wakati, watu wanaokutazama nao watatizama saa, hii ni kwa sababu kuangalia wakati/mda huambukiza.

6. Kunywa maji ya baridi sana mapema asubuhi husaidia mwili wako kufanya kazi vizuri hadi asilimia 25.

7. Kukumbatiana huondoa shauku, msongo wa mawazo na huongeza kinga ya mwili.

8. Kushindwa kumtoa mtu akilini mwako imamaanisha kwamba nawe upo akilini mwa mtu huyo.

9. Watu wenya akili yenye ubunifu hupata shida sana kupata usingizi, hivyo hupendelea kuwa macho hadi usiku wa manane.

10. Kama utakataliwa na mtu ambaye kujali kwake ni muhimu sana kwako, basi maumivu utakayopata katika ubongo wako ni kama maumivu ya mwili yanavyokuwa.

11. Mtu ambaye ametendwa au ameumizwa kisaikolojia huwa na hulka ya kukasirika pasipo sababu yeyote ya msingi.

12. Ukitaka kujua kama mtu unaezumguza nae anapenda kusikia unayoyazungumza kunja mikono yako, kama anapenda na anafurahia mazungumzo nae atakunja mikono pia.

13. Kama mtu anachekacheka tu bila sababu maalumu au anacheka sana, basi mtu huyo ana huzuni kuu moyoni mwake, na kama mtu analala kwa mda mrefu sana, mtu huyo ni mpweke.

14. Namna tunavyozungumza na watoto wetu ndivyo inavyokuwa sauti katika mioyo yao.

15. Mtu akitokea katika ndoto unayoota, basi ni kwa sababu mtu huyo kakuhamu (kakumiss).

16. Wa kwanza kuomba msamaha sikuzote ni mwerevu, wa kwanza kusamehe ni mwenye nguvu na wa kwanza kusahau ni mwenye furaha.

17. Mashairi katika wimbo uupendao ni ujumbe ambao unapambana kuufikisha mahala flani au kuwaambia watu flani.

18. Ukitumia mkono wako usiotumika mara kwa mara (wa kushoto kwa wengi) itakusaidia kuwa na ‘self control’.

19. Kama mwanaume atasimama akiwa ametanua miguu yake wakati akizungumza na mwanamke, ni ishara kwamba mwanaume huyo anampenda mwanamke kwa dhati.

20. Mwanaume akiwa hajisikii huru au akiwa hana amani, basi hushika kichwa au uso wakati mwanamke hushika aidha nywele, hereni, mavazi, mikono au shingo.

21. Siku zote fuata wazo linalokuogopesha zaidi, sababu hili ndili litakalo kujenga na kukuimarisha.

22. Aina mbili ya watu ambao hawatakuangalia machoni: mtu anaejaribu kuficha uongo na mtu anaejaribu kuficha mapenzi/ upendo.

23. Wanasaikolojia wanasema mtu anataka kumfurahisha kila mtu huishia kuwa mpweke zaidi.

24. Mtu anaekasirika kirahisi, kwa vitu vya kijinga, inaonesha kwamba anahitaji upendo/kupendwa.

25. Sikuzote wanaoponda au kulalamikia wengine kwa wanayofanya, ndicho kile wanachofanya wao au wanatamani kufanya wao- elewa hili.

26. Kulia ni afya kwako. Huondoa bacteria wabaya mwilini mwako, hukupunguzia msongo wa mawazo na kukuongezea kinga ya mwili.

27. Saikolojia inasema: Huogopi kupenda, unachoogopa ni kutokupendwa (afraid of not being loved back).

28. Ukweli wa mambo: uko karibu zaidi na kufanikisha malengo yako kama utayaweka kuwa yako pekee, yaani kuwa ni siri yako.

29. Saikolojia inasema: kujifanya mwenye furaha wakati una maumivu ni mfano wa kuonesha ni jinsi gani wewe ni mwanadamu mweye nguvu. (strong person).

30. Kabla ya kulala, asilimia 90 ya akili yako huanza kufikiri mambo ambayo ungependa yatokee.

31. Watu wanaotembea kwa hatua za harakaharaka huonekana kuwa wanajiamini na wenye furaha zaidi kuliko wanaotembea taratibu.

32. Watu wanaojua utani zaidi wanajua kusoma akili za watu pia.

33. Ubongo wa mwanadamu alielala unaweza kuelewa mazunguzo ya watu walio karibu eneo hilo.

34. Ukiwa uaongea na mtu, ongea huku ukitaja jina lake, hii itasaidia kupendwa zaidi na mtu huyo.

35. Kufuatana na uchunguzi wa wataalam, kumtamani mtu kingono hiushia miezi minne, zaidi ya hapo utakuwa ni upendo wa dhati.

36. Uchunguzi unaonesha kuwa watu wanaolala na mito mingi ni wenye msongo wa mawazo na wapweke.

37. Umbo la ubongo wako hubadilika kila unapojifunza jambo jipya.

38. Watu wakiwa katika kundi na ikatokea kuna kucheka, wale walio na mahusiano ya karibu zaidi hutizamana.

39. Kwa namna mwandiko wa mtu unavyokosa mpangilio au kuwa mbaya ndio kiashirio kwamba mtu huyo anafikiri haraka zaidi ya mikono yake inavyoweza kuandika.

40. Kuna watu wana alama ya asili ya kuwaamsha muda wanaotaka, hii ni kwa sababu wana homoni ya asili ya stress.

41. Haiwezekani kukaa na hasira dhidi ya umpendae kwa mda mrefu. Hasira inayofika siku tatu au zaidi inamaanisha kwamba hauna upendo.

42. Chakula cha kwenya ndege hakina ladha sana sababu uwezo wetu wa kutambua ladha hupungua kwa asilimia 20 hadi 50 tukiwa angani.

43. Kama urafiki utafikisha miaka saba, basi urafiki huo utadumu milele.

44. Kama mtu akiongea na wewe halafu kwenye maongezi akakungalia machoni kwa asilimia 60 ya maongezi basi umemboa mtu huyo. Kama atakuangalia kwa asilimia 80 basi umemvutia mtu huyo na kama itafikia asilimia 100 basi mtu huyo anakutishia.

45. Katika sekunde tatu za mwanzo unapoamka, huwezi kumbuka chochote.

46. Uoga waweza kuua. Hii ni kwa sababu mwili huzalisha adrenalin ambayo ni sumu ikizidi. 47. Kawaida, mtu akianza kulia atakumbukaia matukio mengine yaliyomsikitisha au kumchukiza ili kuongezea ubongo wake hamu ya kulia.

48. Unapopiga chafya, unakufa kwa sekunde. 49. Unapotekenywa hucheki, bali ni itikio na kupaniki (panic response). Huwezi jitekenya mwenyewe kwa sababu mwili hauhisi hatari yoyote. Kawaida enzi za zamani kutekenya ilitumika kama adhabu.

50. Kukosa usingizi husababisha ubongo kutokumbuka mambo kiusahihi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad