Maneno ya Jux Kwenye Birthday ya Vanessa Mdee "Swala la Kukupa Furaha Mimi Mwenyewe Nalimaliza Nakupenda Sana"

Maneno ya Jux Kwenye Birthday ya Vanessa Mdee "Swala la Kukupa Furaha Mimi Mwenyewe Nalimaliza Nakupenda Sana"
Kila mwaka ifikapo June 7 huwa ni siku muhimu kwa staa wa kike katika game ya muziki wa Bongofleva Vanessa Mdee, kwani huwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa (Birthday).

Leo June 7,2018 Vanessa Mdee anasherehekea  siku yake ya kuzaliwa akiwa Gabon Brazzavile, Vanessa amepostiwa na watu mbalimbali katika mitandoa ya kijamii kumtakia kheri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.

Jux ameamua kumpost Vanessa na kuandika maneno yanayodhihirisha upendo wake kwa mpenzi wake Vanessa ambaye anasherehekea Birthday yake ya kutimiza miaka 30.

Jux ameandika “Sijui niseme nini kitachoweza kubeba uzito wa thamani yako kwenye maisha yangu @vanessamdee Nitaendelea kumuomba mungu kila siku 🙏🙏 Akupe maisha marefu na afya bora.

“Swala la kukupa furahaa mimi mwenyewe nalimaliza vizuri kabisa Nakupenda sana my love #happybirthday KHAUSA bado naendelea sijamaliza  🎉🎉🎉🎉🎉🎉”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad