Maria na Consolata Kuzikwa Leo Iringa.

Watu wengi wamejitokeza asubuhi ya leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha-RUCU katika ibada maalumu ya kuwaaga pacha waliokuwa wameungana Maria na Consolata waliofariki mwishoni mwa juma.

Miongoni mwa waliofika ni viongozi mbali mbali wa dini na kiserikali.Baada ya ibada kutakuwa na maandamano ya kuelekea katika makaburi ya Tosamaganga ambapo ndipo miili yao itakapo pumzishwa.Vifo vya Maria na Consolata ambao walikuwa ni wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Ruaha vimegusa wengi hasa kutokana na ujasiri walioonyesha wakati wa uhai wao. Vile vile watakumbukwa kwa ucheshi wao.
i.

Kifo chao kiliwagusa wengi Tanzania, wengi wakituma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambaye mapema mwaka huu alikutana na pacha hao, alieleza kusikitishwa kwake na vifo vyao.

"Nimesikitishwa na kifo cha Maria na Consolata. Nilipokwenda hospitali waliliombea taifa. Walikuwa na ndoto ya kulitumikia taifa," aliandika Rais Magufuli kwenye Twitter.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad