Master J: Msanii mkubwa hawezi kumlipa Producer


Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo fleva, Joachim Kimario ‘Master J’ amefunguka kuwa wasanii wakubwa huwa hawalipi pesa kubwa kwa watayarishaji wa muziki kwa kigezo kuwa wanatangaza jina la studio. 

Master J amesema hayo wakati kupitia PlanetBongo ya East Africa Radio, ambapo wasanii wakubwa wanatabia za kuchukua ‘beat’ bure anamwambia producer kuwa anakwenda kumtangaza. 

"Mimi nitasema ukweli leo, Msanii mkubwa hawezi kukulipa hela nzuri wewe 'Producer' atakwambia naenda kukutangazia kwa wasanii underground ambao ndio watakao kulipa", amesema Master J. 

Master J ameongeza kuwa kukosekana kwa ushirikiano baina ya watayarishaji wa muziki ndio chanzo cha wasanii kutoheshimu kazi zao na kupelekea wao kubaki katika hali duni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad