Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha Chadema Tundu Lissu ambaye yupo katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji anatarajia kufanyiwa upasuaji wa 21 wa kuunga goti la mguu wake wa kulia kesho 4/6/2018.
Upasuaji huo ni mwendelezo wa upasuaji wa mwanzo ambao alifanyiwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikokuwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa katika katika makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, 2017.
Lissu ameeleza hayo leo Jumapili Juni 3, 2018 kupitia taarifa aliyoitoa katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram, akiambatanisha na picha yake akiwa amelala wodini kando ya mkewe, Alicia.
"Hello wapendwa wangu. Ninaamini wengi wenu, kama sio wote, mnafahamu kwamba Jumatatu Juni 4 nitafanyiwa operesheni ya mwisho kwenye mguu wa kulia,” amesema.