Moja ya mbinu za kupunguza Mwendokasi kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto barabarani ni kuweka 'humps' maarufu kama matuta kwa wengi. Lakini matuta hayo yanapozidi inakuwa kero
Barabara inayounganisha Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na Tunduma iliyopo mkoani Songwe yenye urefu wa Kilometa 220 ina idadi ya matuta takribani 115, karibia wastani wa tuta moja kila baada ya Kilometa 1
Katika barabara hiyo Kijiji cha Tamasenga kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga peke yake kina idadi ya matuta 10.
Wadau wengi akiwemo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wameonyeshwa kukerwa na matuta hayo na kutaka yaondolewe
Naibu Waziri alisema kuweka matuta kunachangia kuharibu miundombinu ya barabara, pamoja na magari hasa pale magari yapokuwa yakipunguza mwendo ili kupita katika matuta hayo. Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Dk. Halfan Haule amewahi kunukuliwa kuwa wanatumia muda mrefu wa saa 5 hadi 7 kutoka Sumbawanga hadi Tunduma
Nini mtazamo au maoni yako kuhusu utumiaji huu matuta mengi barabarani ili kupunguza Mwendokasi?