Mayweather Aonyesha Jeuri ya Pesa Anunua Saa ya Almasi ya Bilioni 40.2 Sawa na Mshahara wa Pogba na 50 Cent kwa Mwaka Mzima

Mayweather Aonyesha Jeuri ya Pesa Anunua Saa ya Almasi ya  Bilioni 40.2
Mwanamasumbwi Floyd Mayweather ameendelea kujiwekea rekodi zake za kununua bidhaa za gharama zaidi duniani kwani ukiachana na magari ya kifahari anayomiliki, sasa amenunua saa yenye gharama kubwa zaidi duniani.

Mayweather kupitia ukurasa wake wa Instagram ameionesha saa hiyo aina ya  “The Billionaire Watch” na kutaja gharama yake kuwa ni Dola milioni $18 sawa na tsh bilioni 40.2 .

Saa hiyo iliyotengenezwa mwaka 2015 na kampuni ya Jacob & Co inatajwa kuwa ndio saa yenye gharama zaidi duniani kwa sasa na imetengenezwa kwa almasi.

Mayweather amenunua saa hiyo kutoka kwa sonara maarufu zaidi duniani, Mjapani Tadashi Fukushima na kueleza kuwa hawaamini kabisa masonara wengine kwa kile alichoeleza kuwa matapeli.

Kwa gharama ya dola milioni $18 ni pesa anayolipwa kiungo wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba kwa mwaka ambapo yeye analipwa Euro milioni 15.4 hii ni kwa mujibu wa gazeti la Marca .

Kwa upande mwingine, Rapa 50 Cent amemtukana Mayweather kwa kumuita mpumbavu kwa kununua saa hiyo yenye gharama kama hiyo.

“Man they done found the 1 fool in the 🌎 world, dumb enough to buy that watch. LOL🤨get the strap,”ameandika 50 Cent kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Floyd Mayweather buys watch worth $18 million and 50 Cent drags him for it

Top Post Ad

Below Post Ad