Mkufunzi mmoja kutoka chuo kikuu cha Afrika Kusini, anayejulikana kama Dkt.Dyllon Randall amevumbua mbolea inayozalishwa kutokana na mkojo wa binadamu.
Dkt. Randall akizungumza kwenye mkutano na taasisi ya maji ya Afrika Kusini (WISA) amesema kuwa wanachukua kinyesi na mkojo wa binadamu na kuchanganya na maji machafu na kuzalisha mbolea inyojulikana kwa jina ‘new liquid gold- think fertiliser’.
"Mkojo peke yake ni asilimia 1, maji machafu ni asilimia 80 (nitrogen), asilimia 70 ni (potassium) na asilimia 50 (phosphorus) hivi ndivyo virutubisho kwa ajili ya kutengeneza mbolea kutoka kwenye mkojo”, amesema Randall.
Aidha Dkt. Randall ameongeza kuwa sayansi hiyo italisaidia taifa hilo kutokana na hali ya ukame iliyopo, hivyo serikali itatumia gharama ndogo kuagiza mbolea ya nje.