Mboso Awaomba Radhi Basata Kisa Video Yake Chafu

Wikiendi iliyopita msanii kutoka WCB, Mbosso aliposti video chafu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akicheza na mwanamke jukwaani huko mkoani Mtwara alivyokuwa akitumbuiza, video ambayo imepelekea Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) leo Juni 20, 2018 kumuita kwa mahojiano juu ya video hiyo.

Sasa baada ya mahojiano na BASATA, Mbosso amesema kuwa amemalizana na BASATA kwa kuwaomba msamaha kwa yaliyotokea na kuwataka mashabiki wake wamsamehe kwa kuposti video hiyo ambayo watu wengi wameilalamikia kuwa ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

Top Post Ad

Below Post Ad