Mbunge CUF Aiomba Takukuru na Wizara ya Mambo ya Ndani Kumhoji Maalim Sief

Mbunge CUF aiomba Takukuru na Wizara ya Mambo ya Ndani kumhoji Maalim Sief
Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji(CUF) ameiomba Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) na Wizara ya Mambo ya Ndani kumhoji Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Hamad kwa kutopeleka hesabu zinazotakiwa kwa Msimamizi Mkuu wa Hesabu za Serikali.



Khatib amesema kuwa bora mkosoaji huangalia aibu zake kabla ya kusema za wenzake huku akisema kusema mambo hayo kuna hitaji ujasiri.

“Ni mtu ninaye Muheshim Katibu Mkuu wangu, Maalim Seif Hamad lakini katika hili naomba niongee ukweli kwa kweli hajakitendea haki Chama hiki kuacha kupeleka hesabu zinazotakiwa kwa Msimamizi mkuu wa hesabu za serikali , whatever tuna vyombo vinavyoweza kufanya kazi ya kulinda fedha za Chama,” Khatib ameyasema hayo leo Juni 5 Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha mwaka wa fedha 2018/019.

“Naomba sasa TAKUKURU na Waziri wa Mambo ya Ndani ahojiwe Katibu Mkuu kwanini hakupeleka hesabu kwa msimamizi wa hesabu za serikali tuanzie hapo ndio maana tunasema bora ya mkosoaji huangalia aibu zake kabla ya kusema za wenzake, Mh. haya mambo yanataka ujasiri sana,”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad