Mbunge wa zamani wa Kahama, (CCM) James Lembeli, ametangaza kuachana na siasa akitaja sababu kuu mbili.
Lembeli amesema ameamua kuachana na siasa kwa sababu mashirika na taasisi anayofanya nayo kazi, yamemwambia achague moja kubaki kwenye siasa au kuendelea kushirikiana na taasisi hizo.
Lembeli ameyasema hayo leo Juni 13, nyumbani kwake katika kijiji cha Mseki, kata ya Bulungwa, Ushetu, Kahama .
“Hivyo hizi taasisi zimeniambia nichague moja nibaki kwenye siasa au tupige kazi, nimeamua kuacha siasa,” amesema.
Lembeli ambaye alijiunga na Chadema mwaka 2015, amesema sababu ya pili iliyomfanya aachane na siasa ni matatizo yanayoipata familia yake baada ya kujiunga na chama hicho.
“Hapa kwetu kuna kaburi la Mtemi baba yangu. Siku hizi watu wa CCM hawaji kuomba dua kwenye kaburi hivyo nimeamua nisiwe na chama ili watu waendelee kuomba,” amesema.
Ameongezeka: “Napumzika siasa ila mimi bado mchezaji mzuri naamini kila chama nitakachoenda namba yangu ipo tu.”
Chanzo: Mwananchi