Mhasitu Atumia Kanga Kujinyonga Katika Choo cha Baa

Mhasitu Atumia Kanga Kujinyongea Katika Choo cha Baa
Watu wanne wamefariki dunia Mkoani Kilimanjaro, katika matukio tofauti, likiwamo la Mhasibu wa Taasisi ya fedha ya utoaji wa mikopo kwa wakulima na wafugaji (Brac), Victoria Kimario, kujinyonga kwa kutumia kanga katika choo cha Baa moja iliyoko Mkuu Wilaya ya Rombo.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari leo Juni 12, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah, alisema vifo hivyo vilitokea kwa nyakati na maeneo tofauti, Juni 9, mwaka huu.

Akizungumzia tukio la mhasibu wa Brac kujinyonga, Kamanda Issah amesema, tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:45 usiku katika choo cha baa inayojulikana kwa jina la Mgombani iliyoko eneo la Mkuu.

“Choo cha baa ambacho alikutw amarehemu ni jirani na alikokuwa akiishi na uchunguzi bado unaendelea, ili kubaini chanzo cha kujinyonga kwake,”amesema Kamanda Issah.

Katika tukio jingine, kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Bakari(27)mkazi wa kijiji cha Rau River, kata ya Mabogini, amefariki baada ya kujinyonga kwa kutumia shuka la kimasai juu ya mti.

Kamanda alisema kijana huyo ambaye alikuwa dereva wa mitambo ya ujenzi wa barabara, alikutwa amejinyonga kwenye mti jirani na nyumbani kwao Juni 9 mwaka huu.

Wakati huo huo, Fidelis Kimaro,mpakia mizigo (kuli) kwenye magari ya mizigo, mkazi wa Vunjo Mashariki, amefariki dunia baada ya kuruka kwenye gari.

“Mwili wa marehemu ulikutwa pembeni ya barabara kuu ya Arusha-Dar es Salaam, eneo la njia Panda ya Himo, saa 6 mchana na uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa aliruka kwenye gari alipofika maeneo ya nyumbani kwake na gari alilokuwepo lilikimbia na tunaendelea kulitafuta”a,esema

Katika tukio lingine, mwili wa Bakari Anasey (43)mkazi wa Siha  ulikutwa katika mashamba ya Mountain Side ukiwa na majeraha yanayoonyesha kuchomwa na kitu vyenye ncha kali.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad