Serikali nchini Algeria imelazimika kuzima huduma ya Internet nchi nzima kuepuka udanganyifu katika mitihani ya kidato cha sita inayoendelea nchini humo.
Imeelezwa kuwa pia vifaa vyote ambavyo hutumika kupatia huduma ya Internet vimekatazwa kufikishwa katika maeneo ya karibu ambapo mitihani hiyo inafanyika huku mitambo maalumu ikifungwa kubaini uwepo wa vifaa hivyo.
Kwa mujibu wa Serikali huduma hiyo ya Internet itaendelea kukosekana kutokea June 21 mpaka June 25 siku ambayo mitihani itakuwa inamalizika.
Aidha duru za kuaminika zinasema kuwa Serikali hiyo imeamua kuchukua uamuzi huo baada ya mitihani ya mwaka 2016 kuvuja sana kwenye mitandao ya kijamii hivyo wameamua kuzima Internet ili kubana upenyo wa mitihani hiyo kuvuja mitandaoni mwaka huu.