Mke wa marehemu Bilionea, Erasto Msuya, Miriam Mrita ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa iundwe tume ya kuichunguza kesi ya mauaji inayomkabili kwa sababu kuna uonevu unaendelea.
Miriam amewasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba mara baada ya wakili wa serikali, Patrick Mwita kudai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, jalada halisi lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Baada kueleza hayo, Miriam alinyoosha mkono ambapo hakimu Simba alimruhusu kuongea.
Miriam alisimama na kuiambia mahakama kuwa huu ni mwaka wa pili sasa wanaendelea kusota mahabusu.
“Mimi ni mama mjane, mume wangu ameuawa, mimi nipo mahabusu gerezani kwa miaka miwili, kama mama sijui watoto wangu wanaendeĺeaje huko nje.” alionge Miriam.
Aliongeza kuwa amechoshwa na wimbo wa upande wa mashtaka kuwa upelelezi bado haujakamilika.
“Mtu ukishafiwa na mume kuna vurugu mechi zinaendelea huko nje, naomba iundwe tume ya uchunguzi wa kina ya kuichunguza kesi hii kwa sababu kuna uonevu ambao unaendelea.”alieleza Miriam.
Katika kesi hiyo namba 5 ya 2017 mbali na Miriam mwingine anayekabiliwa na kesi hiyo ni Revocatus Muyela.
Kwa pamoja washtakiwa hao, wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada wa marehemu Bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya May 25,2016 huko Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Bilionea Erasto Msuya Ataka Iundwe Tume Kuchunguza Kesi Yake
0
June 04, 2018
Tags