Mlipuko mkubwa katika mkutano wa waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Haijulikani wazi idadi ya watu walioathirika lakini imebidi kiongozi huyo aondoshwe kwa haraka muda mfupi baada ya kutoa hotuba yake.
Maelfu walikuwa wamekusanyika katika bustani kuu ya Meskel mjini Addis Ababa.
Vyombo vya habari nchini vinaripoti kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa na wamepelekwa katika kituo cha afya kilicho karibu na bustani hiyo kupokea matibabu.
Mwandishi wa BBC nchini Ethiopia Emmanuel Igunza aliyekuwa katika eneo hilo anasema kulikuwa na kelele nzito na kubwa iliyosikika karibu na jukwaa walipokaa watumashuhuri muda mfupi baada ya waziri mkuu Abiy Mahmed kumaliza kuuhotubia umati.
Hali ya utulivu sasa imerejea na duru za polisi zinasema wanachunguza tukio hilo.
Umati mkubwa wa watu ulikusanyika katika mkutano huo ulioandliwa kuiunga mkono serikali ya kiongozi huyo mpya anayeidhinisha mageuzi ambayo hayajawahi kushuhudiwa nchini .