Mmiliki mgahawa wa Bunge Apigwa Faini ya Laki 3 Baada ya Kunaswa na Samaki Haramu


Wizara  ya Mifugo na Uvuvi, imekamata samaki aina ya sato (wasiofikia kiwango cha kuvuliwa) kiasi cha kilo mbili kati ya 100 waliokuwa wakiuzwa kinyume cha sheria katika mgahawa wa ofisi ya Bunge jijini Dodoma leo JUmanne, Juni 19, 2018.


Kufuatia tukio hilo, mmiliki wa mgahawa huo, Daniel Lamba, amepigwa faini ya Sh. 300,000 baada ya kukiri kosa la kukutwa na samaki hao wachanga.


Kaimu Meneja wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu wa wizara hiyo, John Komakoma amesema samaki hao ni ambao hawapaswi kuvuliwa kwa mujibu wa kisheria.


“Hawa samaki tumewakamata kwa kuvuliwa kinyume cha sheria, mmiliki wa mgahawa huu amekiri kosa mwenyewe hivyo tumemtoza TSh. 300,000 ambayo atakwenda kulipia benki,” alisema Komakoma.


John Mpepele ambaye ni Msemaji wa wizara hiyo amesema aliyewapa taarifa za kuwepo samaki hao ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyekuja kwenye mgahawa huo jana asubuhi. “Waziri Mpina alipowaona samaki hawa, aliwatilia shaka na kutuagiza kuja kufuatilia,” alisema.


Aidha, mmiliki wa mgahawa huo, Bwana Daniel Labiaramba akikiri kosa kosa amesema; “Nakiri kosa ni weli, lakini katika kilo 100 nilizouziwa, ni ngumu sana kujua iwapo umewekewa samaki hawa, sikufanya hivi makusudi, kwani sikujua,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad