Mobetto Atia Baraka Ndoa ya Lulu "Sina Kinyongo Nikipewa Mwaliko Ntaenda"

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Hamisa Mobeto amebariki ndoa ya staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayetarajiwa kuolewa hivi karibuni na kusema kuwa, hana kinyongo na hata siku ya tukio akipewa mualiko atakwenda.



Akizungumza na Risasi Jumamosi, Mobeto alisema kuwa hana kinyongo na Lulu kama ambavyo watu wanasema kwa kuwa mapenzi yake na mchumba wa Lulu, (bosi wa redio moja maarufu Bongo) yalishakwisha.



“Mimi na huyo anayetaka kumuoa tulishamalizana, hivyo hakuna tena hata chembe ya mapenzi zaidi ya uhusiano wetu wa kulea mtoto.





“Kwa maana hiyo sina shida kusikia Lulu anaolewa na siku ya sherehe nikipewa kadi nitakwenda,” alisema Mobeto. Mobeto na mwanaume anayetarajia kumuoa Lulu waliwahi kuwa wapenzi na kufanikiwa kupata mtoto wa kike aitwaye Fantasy.

Top Post Ad

Below Post Ad