Morocco yagawa dozi, yatuma salam kwa Ronaldo

Kwa mara nyingine vijana wa Herve Renard timu ya taifa ya Morocco wametoa dozi ya mabao matatu kwa moja dhidi ya Estonia.

Juma kaseja amesema anaiamini zaidi timu ya taifa ya Morocco katika michuano ya kombe la dunia kwani ina kocha mzoefu.



Morocco huu ulikuwa mchezo wake wa mwisho ikiwa ni maandalizi ya fainali za kombe la dunia.

Walichokifanya vijana Herve Renard hasa kipindi cha kwanza ni dalili tosha kwamba wana kila uthubutu wa kusema wanakwenda kupambana na kuleta changamoto na sio kama wasindikizaji.

Morocco wapo kundi B – pamoja na hipania, Ureno na Iran. .



Morocco walipata bao la kwanza kupitia kwa Younes Belhanda dakika ya 11 kwa kumalizia krosi ndogo iliyopigwa na Ayoub El Kaabi.

Estonia walinyimwa bao la wazi baada ya Hakim Ziyech kucheza vizuri katika eneo la hatari na kuondosha mpira huo.

konstantin Vassiljev alimjaribu Munir Mohamedi kabla Ats Purje kupiga shuti kali ambalo halikuzaa matunda.

Purje baada alipata nafasi murua na kusiawazishia Estonia.

Hakim Ziyech alifunga bao la tuta kabla ya Nesyri kuhitimissha karamu hiyo ya mabao. Kwa kiwango hiki cha Moroco Ureno na Hispania wanapaswa kuwa makini maana kitumbua kinaweza kuingia mchanga

Morocco watacheza mchezo wao kwa kwanza dhidi ya iran ijumaa ya kwanza ya kombe la dunia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad