Mpinzani Mkuu wa Rais Erdoğan Akubali Matokeo ya Uchaguzi

Mpinzani Mkuu wa Rais Erdoğan Akubali Matokeo ya Uchaguzi
Mpinzani mkuu wa rais Erdoğan,Muharrem İnce ameyapokea na kuyakubali  matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Uturuki.

Muharrem alikuwa akiwania kiti cha urais kupitia chama cha CHP.

Akihutubia katika mji mkuu wa Ankara,Muharram amesema kuwa amekubaliana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa Jumapili usiku.

Rais Erdoğan amechaguliwa kwa mara nyingine kuliongoza taifa la Uturuki.

Ameshinda kwa asilimia 52.2 huku Muharram akiwa na asilimia 30.6.

Vilevile Muharrem amekanusha madai ya kupokea vitisho vya aina yoyote.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad