Mtandao wa Twitter Wapumulia Mashine...Instagram na Facebook Vinara


Katika mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu na inawatumiaji wenye mazungumzo mengi sana ni Twitter, lakini tatizo lake moja kubwa ni kwamba mtandao huu wa kijamii bado hautengenezi pesa za kutosha ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii. 

Mtandao wa Twitter ingawa inavutia mazungumzo mbalimbali kuanzia ya kisiasa, kiutani, n.k yanayohusisha hadi watu mashuhuri kama Rais wa Marekani wa sasa, wasanii na watu wengine mashuhuri kwa wadogo bado mtandao huu unapata shida katika kuvutia makampuni kutumia pesa kujitangaza katika mtandao huo. 

Mtandao wa Twitter bado upo nyuma katika kuvutia mapato yanayotokana na matangazo ukilinganisha na mitandao mingine kama vile Facebook na ata Instagram na Snapchat. 

Katika ripoti ya mapato na ukuaji ya kampuni uya Twitter iliyotoka Alhamisi hii inaonesha bado mtandao wa kijamii wa Twitter unapata shida kukuza idadi ya watumiaji, matangazo na mapato. 

Kwa mfano katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2016 Twitter ilikuwa na wastani ya watumiaji milioni 319 kwa mwezi, huu ni ukuaji wa asilimia 4 tuu ya watumiaji ukilinganisha na kipindi cha mwaka mmoja nyuma, pia namba hii ni ndogo ukilinganisha na mtandao wa Facebook. Facebook ina takribani wastani wa watumiaji bilioni 1.86 kwa mwezi. 

Twitter wanategemea kupata mapato ya dola milioni 91 tuu katika kipindi cha miezi hii mitatu ya mwanzo, hii ni chini sana ukilinganisha na pato la dola milioni 191 ambalo wengi waletegemea wafikie. 

Ingawa bado kibiashara mtandao huo upo katika hali ngumu ila ni uhakika bado hautaenda popote kwa sasa. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bwana Jack Dorsey anasema itaitaji muda mrefu kidogo na mabadiliko kadhaa ili kuweza kuona ukuaji wa watumiaji pamoja na mapato.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad