Mtatiro Asema Hakuna CUF Lipumba Wala Seif

Mtatiro Asema Hakuna CUF Lipumba Wala Seif
Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa Chama cha Wananchi  CUF, Julius Mtatiro amekanusha kuwepo na CUF mbili ndani ya chama chake ambayo hujulikana (CUF ya Lipumba, CUF ya Seif)  kwa madai kuwa Mkutano mkuu wa Chama ulithibitisha kujiuzulu kwa Lipumba tangu 2015.

Akizungumza na East Africa Breakfast, Mtatiro amesema kwamba usaliti alioufanya ndiyo Lipumba umemfanya kutotambulika na vyombo mbalimbali vya Chama hicho, hivyo  kinachofanyika kwa sasa ni Lipumba pamoja 'kagenge' chake kuungwa mkono na Serikali pamoja na Msajili wa Vyama na Chama Cha Mapinduzi lakini siyo  sehemu ya CUF.

Akisisitiza uhalali wa Lipumba ndani ya Chama  hicho, Mtatiro amesema kwamba Msaliti wa ndani huwa hasamehewi popote pale duniani, ndiyo maana wao wanapambana na kiongozi huyo kwa kuwa ni adui wa ndani ya chama.

Mtatiro amesema  kwamba "Lipumba asiitwe upande wa chama kwani madiwani zaidi ya 400 pamoja na Wabunge wa CUF kutoa wale waliotolewa wakawekwa wa CCM wote wanaunga msimamo wa Chama kwamba CUF ipo lakini Lipumba hana upande".

"Unavyostuka nyoka kalala na watoto ndani ya nyumba unamuua haumshiki mkono, lakini kama  ukimuona nje ya uzio wa nyumba yako unamfukuza. Lipumba angekuwa anatusumbua yupo nje ya nyumba yetu tusingehangaika naye, lakini yeye ni adui wa ndani. Wasaliti wa ndani hawasamehewi dunia nzima. Msaliti anayesamehewa ni yule wanje. Ni kam tu vitani. Lakini askari wako wa ndani akienda kuungana na adui haumsamehi. Binafsi siwezi kumsamehe" Lipumba.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad