Kijana mmoja nchini Ubelgiji amefuzu kutoka shule ya sekondari akiwa na miaka 8 baada ya kumaliza masomo yake kwa muda mwaka mmoja unusu tu.
Laurent Simons, ambaye baba yake na mama ni kutoka uholanzi ana IQ ya 145 kulingana na wazazi wake na alipata shahada ya diloma kwenye darasa la wanafunzi wa miaka 18.
Akizungumzana radio na Ubelgiji ya RTBF, alisema somo analolipenda ni hesabu kwa sababu na pana sana.
Baada ya likizo ya miezi miwili atajiunga na chuo kikuu.
Baba yake alisema mtoto huo alipata wakati mgumu akiwa mdogo kucheza na wengine na hakufarahishwa vifaa vya kuchezea.
Laurent anasema alikuwa anataka kuwa daktari wa upasuaji na mwanasayansi wa anga lakini sasa anataka kusomea masuala ya kompyuta.
"Ikiwa ataamua kesho kuwa seremala, hilo halitakuwa tatizo kwetu kama atakuwa na furaha," baba yake alisema.