Mwaka Huu ni Mwendo wa Mijengo...Isabela Mpanda Naye Apewa Mjengo

STORI za kupang­ishiwa nyumba za kishua zimezidi kwa mastaa, weka kando ya Hamisa Mobeto, sasa hivi ni msanii wa muziki nchini, Isa­bela Mpanda naye ameingia kwenye orodha baada ya kupangiwa nyumba nz­ima na mwanaume aliyezaa naye.

Chanzo chetu makini kiliieleza Za Motomoto News kuwa, mwanamama huyo ameham­ishwa kutoka nyumba aliyokuwa akiishi mwanzo na kupelekwa kwenye mjengo kula bata huku mhusika wa jeuri hiyo akitajwa kuwa ni baba wa mtoto wake ambaye ni kigogo wa benki moja jijini Dar.

 Raha ya habari itafitiwe kidogo, ambapo mara baada ya Za Motomoto News kuipata ikaingia kitaa kuisa­ka nyumba hiyo mpya anayoishi Isabela na kugundua kuwa iko Afrikana-Mbezi.

 “Hapa ndipo ninapoishi baada ya baba mtoto wangu wa sasa kunipangishia, siku zote huwa sizai na mwanaume ilimradi bali nazaa na mwanaume mwenye uwezo.”

Top Post Ad

Below Post Ad