Baada ya klabu ya Yanga kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka hapo jana na kufanikiwa kuteua kamati ya kuivusha timu kwenye kipindi cha mpito, timu hiyo imepewa miezi miwili na Waziri Mwakyembe ili ikamilishe uchaguzi wake.
Waziri Mwakyembe ambaye ndiye mwenye dhamana ya Michezo nchini, amewataka viongozi wa Yanga kuziba nafasi zilizowazi ndani ya timu hiyo ili kuhakikisha Katiba ya timu inaendekea kulingwa na kufuatwa vizuri.
''Najua uchaguzi mkuu wa klabu yenu ni 2020 lakini kuna nafasi ambazo zinatakiwa kujazwa hivyo mapengo hayo yazibwe ndani ya miezi miwili sitaki kuona inachukua miezi 9 au mwaka'', aliwaambi viongozi wa Yanga.
Yanga inatakiwa kuziba naasi mbalimbali ambazo zipo wazi ikiwemo ya Mwenyekiti wa klabu endapo aliyekuwa mwenyekiti wao Yusuf Manji hatarejea kwenye nafasi yake. Nafasi zingine ambazo zipo wazi ni wajumbe wa kamati ya utendaji.
Hata hivyo katika mkutano huo wa jana, wanachama kwa pamoja walikubaliana kufanya mabadiliko kisha kuteua Bodi mpya ya wadhamini pamoja na kamati maalum ya kuhakikisha timu inavuka kwenye kipindi hiki cha mpito.
chanzo: EATV