Mwakyembe awasisitiza Yanga kutoichukulia timu hiyo kimzaha


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amewasisitiza wanachama wa klabu ya Yanga kutoichukulia timu hiyo kimzaha na kwamba wanapotetereka msisimko wa michezo pia unakufa kwa kukosa ushindani. 

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu ya Yanga ambapo amewataka wanachama wa klabu hiyokufahamu kwamba klabu hiyo inahistooria kubwa ndani ya nchi ikiwepo harakati za uhuru ndani ya Tanzania. 

"Yanga ikitetereka inaua msisimko, Yanga ikitetereka inaua ushidani wa timu zetu kubwa nchini pia itachangia kuzorotesha maendeleo ya mchezo wa soka sasa ni wajibu wetu sote tushirikiane kukimaliza kipindi hiki cha mpito ndani ya klabu"  Mwakyembe 

Ameongeza kuwa, "Ukiondoa kuleta burudani, lakini pia dhamira yake nyingine ya kuanzishwa kwa klabu hii ilikuwa ni kuleta uzalendo wa kiafrika, Yanga imeshiriki na kuchangia kwenye harakati za uhuru, Muungano na ukombozi wa Bara la Afrika kwa ujumla" 

Katika kutilia msisitizo kuhusu mshikamano katika klabu hiyo Mwakyembe amesema kuwa "Ikifungwa Yanga tunaumia wengi, ndani na nje ya nchi. Yanga ndio alama ya uhuru wa nchi hii. Naamini mkutano wa leo utafanya maamuzi yaliyo sahihi kwa mstakabali mwema wa soka la Tanzania.” 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad