Mwanajeshi wa Kulinda Amani Kutoka Tanzania Ameuawa Katika Shambulio

Mwanajeshi  wa Kulinda Amani Kutoka Tanzania Ameuawa Katika Shambulio

Taarifa kutoka kwa msemaji wa Umoja wa Mataifa leo June 5, 2018 inasema Mwanajeshi mmoja wa kulinda amani kutoka Tanzania ameuawa, katika shambulio lililotokea Jamhuri ya Afrika ya Kati na walinda amani wengine 7 wamejeruhiwa.

Shambulio hilo limetekelezwa dhidi ya kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa wakati kikiwa kwenye doria katika Kijiji cha Dilapoko kilichopo Kusini Magharibi mwa Mji wa Mambere-Kadei.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema inaaminika kuwa shambulio hilo limetekelezwa na wapigani wa Kikundi cha Siriri.

Kati ya waliojeruhiwa mmoja yuko katika hali mbaya anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Bangui huku wengine watatu wakiendelea na matibabu katika mji wa Berberati.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad