Mwanamume Afumaniwa Akijifanya Mwanamke Kuwanyemelea Wanaume Wenzake (Picha)

Mwanamume wa umri mdogo ambaye alijifanya mwanamke ili kuwanyemelea wanaume wenzake kimapenzi amekamatwa Uganda.

Wakati wa mahojiano, alisema alikuwa na mpango wa kupata pesa kutoka kwa wanaume hao. Kulingana na ripoti, alikamatwa alipokuwa akimchezea mwanamume mmoja kwa lengo la kumpora. Iliripotiwa pia kuwa mshukiwa huyo alikamatwa na maafisa wa polisi.

Kwa kutazama picha, mwanamume huyo alikuwa amejimwaya mavazi ya kike pamoja na herini na ‘wig’.

Alikuwa pia amejipaka vipodozi ili aonekane mwanamke kamili. 

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad