Mwanasiasa Maharufu Nchini Uganda Ibrahim Abiriga Auwawa kwa Kupigwa Risasi na Watu Wasiojulikana

Mwanasiasa Maharufu Nchini Uganda Ibrahim Abiriga Auwawa kwa Kupigwa Risasi na Watu Wasiojulikana
Mmoja wa wanasiasa maarufu nchini Uganda Ibrahim Abiriga ameuawa kwa kupigwa risasi jana usiku.


Polisi imesema mwanasiasa huyo wa Chama Tawala cha National Resistance Movement 'NRM' pamoja na mlinzi wake waliuawa karibu na makazi ya mwanasiasa huyo yaliyoko katika eneo linalojulikana Kawanda kaskazini mwa mji mkuu Kampala na watu wasiojulikana.

Abiriga mwenye umri wa miaka 62 ni Mbunge wa Arua na anajulikana kama mmoja wa wanasiasa waliokuwa mstari wa mbele kuunga mkono mswada wa kuondoa ukomo wa umri wa kugombea urais nchini Uganda.

Rais Yoweri Museveni amesema amesikitishwa na kifo cha mbunge huyo na kuagiza maafisa wa usalama kuwasaka waliomuua mbunge huyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad