MWACHIE MBELE YA WATOTO NA UMWAMBIE NA MATUMIZI YAKE, NA WATOTO WASIKIE USIJE KUISHI MAISHA YA UPWEKE UZEENI
MWANAUME
Unamwachia mkeo hela ya Chakula Chumbani, Mke Anatoka na Kapu anaenda kununua Chakula, Anapika, Anawaambia watoto, Njooni Wanangu Mle Nimewapikia Chakula Kitamu, Watoto wakishakula Wanasema Asante Mama.
MWANAUME
Unamwachia Mkeo hela ya Nguo za Sikukuu Chumbani,
Kesho Yake mkeo Anatoka kwenda Kununua Nguo, Akirudi Anawaambia Wanangu Nimewanunulia Nguo za Sikukuu Njooni Mjipimie, Watoto Wakishajipima, Anawaambia Wanangu Mmependeza Eeee, Simnaona Ninavyowapenda
Watoto wanafurahi na Kusema Asante Mama,
MWANAUME
Kila Aina ya Pesa ya Matumizi Unamwachia Mkeo Hela Chumbani,
MWANANUME
Ukifika muda wa kutoa Ada Unamkabidhi Mkeo Hela Chumbani,
Kesho yake Mkeo Anawaambia Watoto kuwa Anaenda kuwalipia Ada ya Shule, Akirudi Anawaambia Wananhu nimeshawalipia Ada, Na gari za Shule Zitakua Zinawapitia, Nataka Msome Wanangu ili Baadae Mje Mnitunze, Watoto Wanasema Asante Mama.
KIBAYA ZAIDI
Ukifika muda wa kutoa Adhabu, Mkeo yeye hatoi Adhabu, Anawaambia Watoto, Ngoja Babayenu Arudi, Nawewe Ukirudi Unaelezwa na Mkeo matatizo ya Wanao, Unachukua Bakora Unawaadhibu Watoto, Bila kujua kuwa Unazidi Kujenga Uhusiano M'BAYA na Wanao.
NGUMU KUMEZA
Ukifika Uzeeni, Watoto wako Hawana KUMBUKUMBU Yoyote Ya Mema Uliyowafanyia.
NA
UKUMBUKE KUWA-->>
MTOTO ANAANZA KULISHWA SUMU YA MANENO KUTOKA KWA MAMAYAKE KUANZIA UMRI WA MIAKA 9 --- 15
MWANAUME KUWA MAKINI SANA
ZINGATIA HAYO KWA MAISHA YA UZEENI