Katika Ajenda namba 5 iliyokuwa imewekwa kwa ajili ya kujadili barua ya aliyekuwa Mwenyekiti wao, Manji aliyoituma akitaka kujizulu, imepingwa na wanachama wote wa ujumla huku wakisema kuwa anafaa kuendelea kuwa Mwenyekiti.
Kutokana na maamuzi ya wanachama hao, Mzee Akilimali amekuja kivingine na kupinga maamuzi hayo akisema si jambo la kawaida kwa Manji kuendelea kuiongoza Yanga kwakuwa hakuna na timu kwa takribani mwaka mzima.
Mzee huyo ameeleza haiwezekani Manji akaendelea kuwa Mwenyekiti Yanga ilihali hajaweza hata kuwasili kwenye mkutano mkuu kuja kutoa hata sababu za kwanini aliamua kutuma barua hiyo.
"Haiwezekani mtu amekaa pembeni kwa takribani mwaka mzima halafu leo mnatoa maamuzi ya kutaka aendelee kuiongoza Yanga!! Kwanini asingeweza kuja hata kwenye mkutano akatoa sababu au hata kuomba radhi? Mimi sikubali" alisema.
Jumla ya wanachama wote 1400 wlaohudhuria mkutano huo wamepinga barua hiyo na wameridhia kuwa Manji ataendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo.