Nabii Nchini Nigeria Ataka Milion 4 Kuisaidia Nigeria Kushinda Kombe la Dunia


NABII NCHINI NIGERIA ATAKA MILLIONI 4 KUISAIDIA NIGERIA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA 2018:
Nabii wa kujitawaza nchini Nigeria anayejulikana kama Tommy Yisa Aika amewataka waumini wake wamlipe kiasi cha naira 750,000 sawa na zaidi ya Milioni 4 za Kitanzania ili atume kikosi chake cha mashujaa wa maombi kiwasaidie timu ya taifa ya Nigeria kushinda kombe la dunia nchini Urusi.

Kwa upande mwingine Nabii huyo alisema kuwa timu hiyo ya taifa ya Nigeria ilipokea kichapo kutoka kwa Croatia kwa sababu Mungu alikuwa anaawadhibu kwa kumchagua kocha mzungu ambaye ni Gernot Rohr.

Katika mechi hiyo Nigeria walichapwa 2-0 na Croatia ambayo ndio ilikuwa mechi yao ya kwanza katika Kombe la Dunia Urusi.

Aidha Nabii huyo amesema kuwa waumini wake maalum wako tayari kuanza kazi na kurekebisha kosa walilolifanya na kupata neema ya Mungu katika michuano hiyo.

Nigeria watakutana na Argentina katika mechi yao ya mwisho Kundi D na ndio itakayoamua hatma ya timu hiyo kusonga mbele katika michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad