TCRA inawataka wachapishaji wa maudhui katika blogu na majukwaa ya mtandaoni kujisajili na kupata leseni kulingana na gharama zilizoanishwa.
Baadhi ya mitandao ikiwemo Jamii Forum imesitisha huduma hizo kutokana na tangazo la TCRA linalosema ni kosa kisheria kutoa huduma ya maudhui ya mtandaoni bila kuwa na leseni, hivyo kuanzia Juni 11, 2018 watoa maudhui hawaruhusiwi kuweka taarifa mtandaoni.
Nape aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter huku akiambatanisha picha ya mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo amesema,
“Hili la JF (Jamii Forum) linafikirisha. Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza kutana nao..... kimya kimya!."