Nape Afunguka Baada ya Mtandao wa Jamii Forum Kufungwa

Kitendo cha Mtandao wa Jamii Forum kufungwa na Mitandao mingine ya Kijamii nchini kutokana na kanuni za maudhui ya kimtandao za mwaka 2018, kimemuibua Mbunge Mtama Nape Nnauye ambapo amefunguka na kutoa maneno mazito.

TCRA inawataka wachapishaji wa maudhui katika blogu na majukwaa ya mtandaoni kujisajili  na kupata leseni kulingana na gharama zilizoanishwa.

Baadhi ya mitandao  ikiwemo Jamii Forum imesitisha huduma hizo kutokana na tangazo la TCRA linalosema ni kosa kisheria kutoa huduma ya maudhui ya mtandaoni bila kuwa na leseni, hivyo kuanzia Juni 11, 2018 watoa maudhui hawaruhusiwi kuweka taarifa mtandaoni.

Nape aliyewahi kuwa Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter huku akiambatanisha picha ya mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo amesema,
“Hili la JF (Jamii Forum) linafikirisha. Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza kutana nao..... kimya kimya!."
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad