Mbunge Mtama, Nape Nnauye amejikutaka akijibu hoja mbali mbali mtandaoni kufuatia mtandao wa Jamii Forums kusitisha kutoa huduma.
Jamii Forums wamefikia hatua hiyo kutokana na kanuni za maudhui ya kimtandao za mwaka 2018.
Sasa Nape Nnaye alianza kueleza hisia zake kuhusu hilo kwa kuandika kwenye mtandao wa twitter; "Hili la JF linafikirisha! Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza Kutana nao….. kimya kimya!."
Baada ya tweet hiyo idadi kubwa ya wachangiaji walionekana kumnyooshea kidole kutokana kipindi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipitisha sheria ya huduma za vyombo vya habari kwa mwaka 2016
Hata hivyo Nape aliwataka wachangia kutofautisha vitu hivyo kwani ni sheria mbili tofauti.
Baada ya kubishana nao tangu jana hadi leo mchana, Nape aliamua kunyoosha mikono juu na leo saa 8 mchana akaandika katika akaunti yake ya twitter akisema:
“Nilaumuni kwa ‘bao la mkono’ lakini sio kwa hili la JF”
Baadaye aliandika tena akisema: