Natamani Ngasa Arudi Yanga - Cannavaro


Aliyekuwa Nahodha wa timu yaTaifa Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye kwa sasa ndio Nahodha wa klabu ya Yanga amefunguka kuwa anatamani kumuona Mrisho Ngasa anarudi kuichezea Yanga.


Akizungmza  kwenye kipindi cha KIKANGONI,kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Cannavaro amesema ngasa ni mchezaji mzuri na amefanya mambo mengi ndani ya klabu ya yanga.

Cannavaro amesema ngasa ameisaidia yanga kwa namna moja au nyingine kwahiyo kama akirudi matumaini ni kufanya vizuri zaidi katika klabu.

“Ngasa ni mchezaji mzuri sanaa na amefanya vitu vingi ndani ya timu ya Yanga kwa hiyo natamani arudi hata leo kwa kuwa ni mkali katika mchezo, akirudi ataendelea kufanya vizuri zaidi ndani ya klabu”, amesema Cannavaro.

Ameongeza kwa kutoa ufafanuzi kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, “mtu kama Cristiano Ronaldo timu yake inamtegemea sanaa ndani ya timu yeye ndio kila kitu lakini mtu kama Lionel Messi ndani ya timu hategemewi sanaa kwa kuwa ndani ya timu yake kuna wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa kama yeye".
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad